Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea mfano wa funguo yenye ujumbe wa "Mabadiliko", kutoka kwa Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini Septemba 14, 2015.
Sehemu ya Umati wa wananchi wa Mji wa Kahama, wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini l Septemba 14, 2015, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.