Moto uliozuka katika mlima wa Meru siku tatu zilzopita bado umeendelea kuwaka huku jitihada mbalimbali za udhibiti zikiendelea kwa ushirikiano baina ya shirika la hifadhi za taifa nchini na wananchi wa vijiji vya jirani.
Akizungumza mazingira ya moto huo katika eneo la tukio meneja mawasiliano wa Tanapa Pascal Shelutete anasema chanzo cha moto huo ni shughuli za binadamu wakiwemo watu wanaowasha moto kwa ajili ya kurina asali.
Hata hivyo Tanapa inawatoa hofu wananchi wa Arusha na maeneo ya jirani kuhusu taarifa zilizoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa moto huo umesababishwa na mlipuko wa volkano.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nasari aliyefika eneo la tukio kushirikiana na wananchi kudhibiti moto huo anatoa wito kwa wananchi kuendeela kujitokeza na nguvu kuongezwa ili kunusuru rasilimali hiyo muhimu kwa maisha ya wananchi na utalii.