Ommy Dimpoz apagawishwa na jimama jukwaani

Mwanamuziki Ommy Dimpoz, amejikuta akipagawa baada ya mwanamke mmoja kumwagia fedha ambazo sio chini ya laki moja na kuamua kumhonga hadharani alipokuwa anatumbuiza jana katika uzinduzi wa ‘Amerudi’ Mango garden jijini Dar es Salaam.
Katika hali ya taharuki mwanamke mmoja alipanda jukwaani na kuanza kummwagia fedha hizo Dimpoz, wakati akiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa ‘Nani kama mama’ na hivyo kushindwa kuzuia hisia zake kwa mtunzaji huyo.
Ommy Dimpoz, alionekana kuishiwa cha kusema na kuwauliza mashabiki wake ampe zawadi gani mwanamke huyo ambaye ameonesha kutambua mchango wake na ndipo washabiki waliporopoka kuwa aondoke naye, na yeye kwa heshima alionesha ishara ya kumshukuru mama huyo na kumpa kofia yake kama zawadi na kumvalisha na ukumbi kukuzima kwa furaha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo