Baraza la habari Tanzania (MCT) limeanza kutoa mafunzo maalumu wa waandishi wa habari yatakayowajengea uwezo wa kuandika habari sahihi zinazohusiana na masuala ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi OCTOBA zitakazowapa wananchi uwezo wa kuwapima wagombea na hatimaye kuchagua viongozi wenye sifa.
Hayo yamesemwa leo na ALAKOK MAYOMBO, afisa program mwandamizi wa MCT anayeshulikia masuala ya viwango na ubora wakati akielezea madhumuni ya mafunzo hayo yanayowashirikisha waandishi wa mikoa ya MWANZA, GEITA, SIMIYU, KAGERA na SHINYANGA yatakayochukua siku TANO.
Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, CHRIZOSTOM RWEYEMAMU katika ufunguzi wa mafunzo hayo amewahimiza waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli ili wajiepushe madhara ambayo wanaweza kukumbana nayo
Nao MBEKI MBEKI na ROSE SAMWEL ambao ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo wanaoeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kuandika habari zinazohusiana na masuala ya uchaguzi, huku MIDRAJI IBRAHIMU akiwaomba wamiliki wa vyombo vya habari wawawezeshe waandishi ili wajiepushe na vitendo vya uandishi wa habari usiozingatia maadili.
Mafunzo hayo yamegawanywa katika mikoa iliyoko kwenye kanda SABA ambapo jumla ya waandishi MIA MOJA SABINI na TANO hapa nchini watanufaika na mafunzo hayo.