Ndesamburo amfuata Dkt Willbroad Slaa nyumbani kwake

ALIYEKUWA Mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Wilbroad Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa jimbo hilo, Japhary Michael.
 
Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA. Mgombea mwenza aliyeteuliwa ni Mh. Juma Duni Haji.  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo