Mbunge afa kwa ajali ya gari

Clara Mwatuka enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Clara Mwatuka, amefariki dunia Jumapili jioni baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuelekea Ndanda, Masasi mkoani Mtwara.
mwatuka gari
Gari alilopata nalo ajali marehemu Mwatuka.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake, ambaye inasemekana ni mwanaye. 
Mwili wa marehemu Mwatuka umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda. 

Viongozi waandamizi wa CUF wamethibitisha kutokea msiba huo.
wenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo