Kuhusu kumpa mtu kadi yako ya kupigia kura, soma maelezo haya

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeonya kwamba mtu yoyote haruhusiwi kutoa kadi yake ya kupigakura au taarifa za kadi hiyo kwa ndugu, jamaa au mwajiri wake.
NEC imetoa onyo hilo wakati tayari kukiwa na tetesi kuwa baadhi ya wafanyakazi wa umma wakiwamo polisi, wanajeshi na askari magereza wametakiwa kukabidhi kadi zao kwa viongozi wao wa ngazi za juu.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika jana aliitisha mkutano wa Vyombo vya Habari akidai kuna tetesi Serikali imeviagiza vyombo vya usalama, kupeleka namba za vitambulisho vya askari wote kwa wakuu wa vitengo jambo ambalo ni kunyume na utaratibu
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Kombwey amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ambayo inazungumzia Daftari la Kudumu la Wapigakura, hairuhusiwi na haitakiwi kwa mtu asiyehusika na kadi ya mpigakura kuimiliki kadi hiyo.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga alisema taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote kuwa wanajeshi wameombwa nambari za vitambulisho na Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba alipopigiwa simu kuhusu madai hayo, alisema hana hizo taarifa, huku Ofisa Mawasiliano wa Magereza, Deodatus Kazinja alisema hizo ni tetesi na wala hazina ukweli wowote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo