MABWENI matano katika shule tano za upili katika kaunti ya Kilifi yalichomwa usiku wa Jumanne katika kisa kilichoduwaza wengi.
Mabweni hayo yalichomwa katika usiku mmoja katika kile ambacho maafisa wa elimu na polisi wanaamini kilipangwa na wanafunzi wahuni.
Kati ya mabweni matano ambayo yalichomwa, matatu yaliharibiwa kabisa huku mengine mawili yakiokolewa kabla ya kuchomeka kabisa. Kiini cha moto huo bado ni kitendawili huku polisi na wakuu wa elimu wakiamini kilitekelezwa na wanafunzi wahuni.
Shule ambazo mabweni yao yalichomeka kabisa ni Chumani, Dzitsoni na Lutsangani.
Kulingana na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Kilifi Bw Dickson Ole Keis, jaribio la wahuni hao kuchoma shule ya upili ya Chasimba na Jaribuni hazikufua dafu kwani walizuiwa na walinzi wa usiku.
Hali ilikuwa hivyo katika shule ya upili ya Jaribuni ambapo walichoma magodoro manne na vitanda viwili.
Msimamizi wa polisi katika eneo la Kilifi Bw Joshua Ole Leina alisema kuwa kisa cha kwanza kiliripotiwa katika shule ya upili ya Dzitsoni
“Tunaamini kwamba visa hivi vya kihuni vilipangwa na wanafunzi wenyewe.”
