Picha: Vijana 30 wa vyuo vikuu wa CCM wahamia CHADEMA

Vijana 30 wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamerudisha kadi za CCM katika Tawi la chama cha (CHADEMA) Mwananyamala kwa madai kuwa hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombe wa urais wa CCM.Siku chache baada ya kumalizika kwa mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya urais ndani ya CCM, mgawanyiko ndani ya chama hicho umeeanza baada ya uwepo la wimbi kubwa la wanachama kuanza kukihama huku zaidi ya vijana 50 wakijiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.

Sasa ni rasmi, Bw Maiko Litanda aliyekuwa kiongozi wa kundi la M4U, lililokuwa likimuunga mkono mbunge wa Monduli Edward Lowasa anasema maamuzi yaliyofanywa kwa manufaa ya wachache ndani ya CCM kwa kumkata jina Bw Edward Lowasa wanasema hawakati tamaa na kwamba safari yao ya matumaini bado inaendelea na sasa inahamia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.
 
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa M4U anasema zaidi ya viajana 100 wamekwisha kujiunga na Chadema ambapo blog hii imeshuhudia kadi 50 pekee za vijana hao, huku uongozi wa Chadema mkoa ukiwahakikisha kuwafikisha salama katika safari ya matumaini.
 
Katika hatua nyingine chama cha ACT wazalendo kimepokea wanachama 7 kutoka vyama vya upinzani ambapo wanadai kuondoka kwao kunatokana na viongozi wa vyama hivyo kuwa na ombwe la uongozi huku vingine vikiendeshwa kwa ukanda.
 
Vugu vugu hili linakuja siku kadhaa zikiwa zimesalia kabla ya Ukawa kumuweka wazi mgombea wao wa urais huku kukiwa na hatihati huenda mmoja wa vigogo wa CCM yuko mbioni kujiunga na umoja huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo