Kikao cha UKAWA kilichokaa leo na kujumuisha Wenyeviti na makatibu wakuu wanaounda vyama hivyo, wamefikia makubaliano.
Mambo makubwa waliyokubaliana UKAWA ni ugawanaji wa majimbo ya Ubunge na kusimamisha mgombea mmoja wa Urais atayetangazwa leo.
Kwakuwa UKAWA si chama cha siasa, mgombea huyo wa Rais anatolewa ndani ya chama kimojawapo na ataungwa mkono na vyama vyote.
Prf. Ibrahim Lipumba amesema kuwa kuna mambo machache wanamalizia na baadaye leo hii watamtangaza rasmi mgombea Urais wa UKAWA
Mambo machache wanayomalizia kukubaliana UKAWA, Prof. Lipumba amesema ni mambo madogo ambayo hayawezi kuleta matatizo yoyote
