Makubwa: Wafanya sherehe kufurahia waziri Membe "kukatwa" na CCM

Baadhi ya wnaanchi wa jimbo la Mtama, lindi wamejikuta wakikesha na kufanya sherehe usiku kucha wakifurahia kushindwa kwa Mbunge wao Benard Membe katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais.
Furaha za wananchi hao ziliibuka baada ya kupata taarifa ya kushindwa kwa Membe katika mchakato wa mbio za Urais.
Baadhi ya wananchi hao walioonyesha furaha yao waziwazi walichinja wanyama wakiwemo ng’ombe na mbuzi idadi isiyopungua kumi,kupika chakuna na kuserebuka kwa muziki.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananachi hao walisema wameyapokea matokeo hayo kwa furaha kubwa kutokana na kushindwa kushirikiana na wananchi wake kuwaletea maendeleo na kupunguza kero zinazowakabili ikiwemo kero ya maji, miundombinu ya barabara na afya.
Wamesema hawatamsahau Membe kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake alizokuwa akizitoa kwao wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wao
chanzo:gazeti la sema usikike


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo