KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE MAKETE, WAGOMBEA WATOANA JASHO JUKWAANI

Mbunge wa Makete aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge akiomba kura kwa wanachama wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoani Njombe ya kuteuliwa kwa awamu nyingine kuwa mbunge wa jimbo la Makete. Mbali na kuomba kura lakini mgombea huyo ameeleza aliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitano 2010-2015 wakati akiwa madarakani, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara, umeme, maji, elimu n.k, na kusema pia ametoa kitabu chenye kuelezea mambo yote aliyoyafanya akiwa madarakani.Dkt Mahenge akiendelea kujieleza wakati akiomba kura.
 Mgombea kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Makete kupitia CCM Bw. Fabian Nkimwa akiwaomba kura wananchi ili ateuliwe kuwa mgombea rasmi wa ubunge wakati akijinadi kwa wananchi wa kata ya Tandala. Mgombea huyu pamoja na mambo mengine amewaomba wananchi waepuke kuwachagua wagombea wanaotoa fedha ili wachaguliwe.
Mgombea aliyejitambulisha kwa jina la Lufunyo Nkinda akiomba kuchaguliwa ili apate ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine amesema akiingia madarakani atatekeleza ilani mpya ya CCM pamoja na kusukuma ilani ya sasa iliyosuasua kutekelezwa, hasa akiitaja barabara ya Njombe - makete kujengwa kwa lami
 Mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Makete Prof. Norman Sigala King akiomba kura katika viwanja vya lishe MTC Tandala ili awe mgombea pekee wa CCM kugombea ubunge wa Jimbo la Makete katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutoa msuumo katika elimu kwa kukiboresha chuo cha ualimu Tandala pamoja na miundombinu hasa barabara ya lami Njombe - Makete
 Dkt Norman akijinadi

 Wananchi wa Tandala wakifuatilia sera za watia nia hao (Picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo