Jerry Muro apasuliwa nazi wakati akijinadi kwenye kampeni za Ubunge

Kumekuwa na wimbi la watu maarufu kuingia katika siasa na kutangaza kugombea nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwezi Oktoba 2015.
Jerry Muro ni mmoja kati ya watu maarufu waliojitokeza kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM.
IMG-20150730-WA0012Kama ilivyo kawaida kwa chama chochote cha siasa wagombea huwa wanajinadi mbele ya wanachama wa chama husika na kuomba kura, Jerry alipata mkasa ambao mwenyewe anakiri kumtisha. Jerry ambae anaomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge kwa jimbo la kawe kwa tiketi ya CCM anapata upinzani kwa watiania 20.
IMG-20150730-WA0011July 30 Jerry Muro akiwa  katika kata ya Msasani Bonde la Mpunga wakati anajinadi walitokea vijana wawili, mmoja akavunja nazi na mwingine akavunja mayai vitu ambavyo vinaashiria imani za kishirikina, Jerry amekiri hali hiyo kumtisha maana mambo hayo amekuwa akiyasikia na sio kuyashuhudia.
“Nimepata athari kwa kiasi kikubwa kwa mfano leo tumekwenda katika kampeni nilipoanza kujieleza nimemwaga sera wakatoka watu wawili mmoja akapasua nazi mwingine akapasua mayai”>>> Jerry Muro
Jerry Muro ameingia katika gumzo ya kuwa mmoja kati ya watu maarufu waliotangaza kugombea Ubunge Jimbo la Kawe ambalo mbunge wake wa sasa ni Halima Mdeekutokea CHADEMA.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo