HALMASHAURI YA NJOMBE YAGAWA MAMILIONI YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI


Halmashauri ya Mji Njombe imetoa msaada wa fedha wenye thamani ya shilingi Million tano (5,000,000/=) kwa vikundi vya Wajasiriamali vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU), ambapo fedha hizo zitatumika 

kuendeleza miradi mbalimbali iliyoanzishwa na iliyopendekezwa kuanzishwa 
na vikundi hivyo.


Mratibu wa Ukimwi katika Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Daniel Mwasongwe alisema, fedha hizo zimetolewa kwa lengo la kuviwezesha vikundi hivyo kuongeza kipato ambacho kitawasaidia kuendesha maisha yao
ya kila siku, kuondokana na dhana ya utegemezi na kuimarisha umoja na 

mshikamano miongoni mwa wanakikundi.


“Halmashauri ina vikundi vingi sana vya WAVIU ambavyo vinahitaji misaada 

kama hii ili kuweza kukuza na kuendesha miradi yao. Lakini leo hii 

tumeamua kutoa msaada huu wa fedha kwa baadhi ya vikundi kutokana na 

ukweli usiofichika kuwa miradi yenu ipo wazi na inaonekana. Tumieni fedha 

hizi kuendeleza miradi ambayo ni endelevu na ambayo mmeridhia kuianzisha 

kama kikundi. Tutafika na kukagua ni hatua gani mmepiga baada ya kupokea 

msaada huu.”Alisema mratibu huyo


Jumla ya Vikundi 6 vya WAVIU kutoka katika Kata tano ndani ya Halmashauri 

ya Mji Njombe vimenufaika na Msaada huo. Vikundi hivyo ni pamoja na 

Kikundi cha Matumaini kilichopo Kata ya Uwemba ambacho kilipewa fedha 

Taslimu shilingi 800,000/= kwa ajili ya shughuli za ufugaji nyuki na kilimo 

cha viazi, Kikundi cha Muungane kutoka Kata ya Uwemba ambacho kilipewa 

fedha Taslimu shilingi 1,000,000/= kwa ajili ya shughuli za Ufugaji nyuki na 

Kilimo cha viazi, Mwongozo kutoka kata ya Njombe Mjini ambacho kilipewa 

shilingi 800,000/= kwa ajili ya Ufugaji Kuku wa Kienyeji, Tulindane kutoka 

Kata ya Kifanya Shilingi 800,000/= kwa ajili ya Ufugaji Nyuki, Kikundi cha 

Upendo kutoka Kata ya Mji Mwema Shilingi 600,000/= kwa ajili ya Upandaji 

Miti na Kikundi cha Twitange kutoka Kata ya Matola Shilingi 1,000,000/= 

kwa ajili ya Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa.


Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri ya Mji Njombe ameiomba jamii, Asasi za 

Kiserikali na Zisizo za Kiserikali kujitokeza kuvisaidia vikundi hivi vya WAVIU 

kwa kuwapatia misaada mbalimbali popote pale Nchini na kuondokana na 

dhana ya Kuwanyanyapaa na kutotambua mchango wao haswa katika 

maswala ya Kiuchumi na Ujasiriamali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo