Ajali mbaya imetokea leo majira ya saa nane mchana ikihusisha treni na basi la abiria huko mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea eneo la Mororo,Tabora. Inasemekana watu watu ambao idadi yao haijajulikana wamepoteza maisha kwenye eneo la tukio.
Lakini taarifa zilizoripotiwa na kituo cha redio VOT Tabora ni kuwa ajali hiyo Imetokea mkoani Tabora barabara ya kwenda Urambo umbali wa kilomita kama kumi hivi kutoka Manispaa, baada ya gari la abiria kugongana na treni ya mizigo kwenye "Railway crossing", watu waliofariki bado hawajafahamika idadi yao kamili ila waliotambuliwa ni wawili mmoja ni Samweli, mkazi wa kata ya Ufuruma wilayani Uyui na Mwingine ni Issa
taarifa zaidi zitakujia hapa hapa