Angalia Kituo feki cha Polisi.. Kina kila kitu ila feki !!

Fake
Pata picha mtu anajiamini kabisa anaanzisha Kituo cha Polisi, anafanya kila kitu kama Polisi wanavyofanya.. kuna pingu, sare za Askari, Silaha… unaambiwa mpaka gari yake ina king’ora juu kama gari ya Polisi kabisa, lakini kila kitu ni feki na jamaa amepiga kazi kwa miaka miwili hakuna aliyemshtukia Kituo hicho feki cha Polisi.
Ishu ilikuja kushtukiwa baada ya mpenzi wake na jamaa huyo kuamua kuripoti Polisi kwenyewe, jamaa wakamfatilia mpaka wakamkamata.Mchina huyo anajiita Lei, alikorofishana na mpenzi wake, katika majibizano yao ikaonekana jamaa anatishia kuisambaza mitandaoni video inayoonesha wakiwa wanafanya mapenzi.. mwanamke akaona isiwe tatizo, akaenda moja kwa moja Polisi kuripoti.
Lei alikuwa akifanya mishemishe zake hizo Jimbo la Hubei China kwa muda wote mpaka alipokamatwa, jinsi ambavyo alijikamilisha wapo ambao aliwahi kuwakamata kabisa na kuwatoza faini ili mambo yaishe juujuu, mwishowe amekutana na Polisi wenyewe… stori za kukamatwa kwake zimechukua sana headlines mitandaoni, wengi wamejiuliuza imekuwaje akafanya kazi yake feki miaka miwili bila kukamatwa?
POLICE FEKI II


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo