Aliyekuwa mtia nia urais CCM aomba kurudishiwa pesa zake za fomu, la sivyo ataifikisha CCM mahakamani

Kada wa Chama cha Mapinduzi Dk.Musa Muzamili Kalokola aliyekuwa akiomba ridhaa ya kuomba kugombea nafasi ya Urais ametoa kituko baada ya jana kutaka arudishiwe fedha yake milioni 1 aliyochukulia fomu.
Kalokola ambaye alikuwa miongoni mwa makada 42 wa CCM waliochukua fomu za kuomba kuwnaia Urais, amesema hakubaliani na mchakato wa kumapata mgombea wa CCM ulivyokwenda, kwani wagombea hawakupewa fursa ya kujieleza , hivyo anataka arudishiwe fedha zake.
Alisema utaratibu ulikuwa wa hivyo na kwamba inashangaza wagombea kutolewa fursa ya kujieleza mbele ya wajumbe.
“Sikubaliani na mchakato ulivyokwenda hata kidogom hivyo nitaandika demand notisi wanirudishie fedha zangu walizochukua na nilizotumia kuzunguka kutafuta wadhamini,”Kalokola.
Alipoulizwa kama atamuunga mgombea aliyepitishwa na CCM kuwania nafasi ya Urais alisema kuwa kila mtu atabeba msalaba wake.
kitenge


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo