MTUHUMIWA WA UJANGILI SIMIYU ALIYETOROKA "KIUTATA" AKAMATWA AKIWA MAFICHONI

Jeshi la polisi mkoani simiyu kwa kushirikiana na kikosi maalum cha askari wa hifadhi ya taifa ya Serengeti  wamefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa ujangili  bw madeni nindwa mkazi wa kijiji cha mwalukonge wilayani busega aliyekamatwa na meno ya tembo yenye thamani shilingi milioni 17,baada ya kutoroka na hatimaye  kukamatwa katika kijiji cha makomero wilayani igunga alikokuwa amejificha.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa simiyu ssp jonathan shana amesema kuwa kesi hiyo ilifunguliwa ,katika mahakama ya wilaya ya magu  ec2/2014 mbele ya hakimu masige ambapo iliendeshwa siku tatu mfulilizo  kuanzia,desemba 2 hadi desemba 5,2014 na kumalizika kusikilizwa na mtuhumiwa alijitetea januari,8,2015 na kubaki hukumu dhidi yake.

katika mazingira ya kutatanisha mtuhumiwa januari 13 mwaka huu, alitolewa gerezani kwa removal order iliyosainiwa na hakimu aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo bila kuwepo kwa wakili  mwandamizi mfawidhi wa wa serikali .

Shana amesema jalada la uchunguzi limefunguliwa kupata ukweli wa mazingira kwa mtuhumiwa kuachiliwa mahakamani huku akitoa wito kwa wananchi.

Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakama ya wilaya ya magu ,juni 22 ili kujulishwa hukumu iliyotolewa dhidi yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo