Mbunge wa CCM atishia kuchukua maamuzi magumu edapo jina lake litakatwa ili asigombee tena

Mbunge wa CCM jimbo la Korogwe vijijini mheshimiwa Stephen Ngonyani ametishia kuchukua maamuzi magumu kwa madai kuwa baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho wanakusudia kuondoa jina lake katika kikao cha uteuzi wa nafasi hiyo cha halmashauri kuu ya CCM kwa madai kuwa yeye sio mzaliwa wa jimbo hilo.

Ni msafara wa makundi ya vijana wa Korogwe mjini waliokuwa wamekwenda kumpokea mbunge wao ambaye alikuwa nchini India kwa matibabu kisha kuhutubia wananchi kuhusu kampeni inayofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM kuwa mbunge huyo sio mzawa hatua ambayo amesisitiza kuwa inaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama endapo atachukua maamuzi magumu.
 
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa umoja wa vijana (UVCCM) wilayani Korogwe wamesema wataunga mkono maamuzi yoyote yatakayotolewa na mbunge wao hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika endapo maamuzi hayo yatachukuliwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo