Linahesabika kama tukio jingine la Basi kuwaka moto katika rekodi za mabasi yaliyowaka moto yakiwa safarini nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu ni kwamba basi hili la kampuni ya Dar Express liliwaka moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa abiria.
Amesema >>> ‘Ni kweli basi la Dar Express saa saba mchana kwenye kijiji ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima, hakuna yeyote aliejeruhiwa‘