Mtoto mchanga wa kiume wa siku tatu katika mtaa wa Masanga Wilaya ya Igunga ameokotwa akiwa amekatwa viungo vyake na watu wasiojulikana.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Masanga Julius Kitundu alisema mtoto huyo aliokotwa na wasamaria wema pembezoni mwa barabara ya lami.
“Kwa kweli kitendo kama hiki kimetusikitisha na watu waliofanya kitendo hicho wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kufikishwa kwenye vyombo husika” Kitundu.
Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuwaomba watoe ushirikiano kwa jeshi la Polisi katika kuwasaka wahusika.
Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo hicho cha kinyama na kusema wataanzisha msako mkali ili kuhakikisha waliohusika wanakamatwa na mama aliyejifungua anashikiliwa.