Msichana Judithi Chomile (15) amekiri kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa shule ya msingi Bernard Benderi aliyejulikana kwa jina la Edrini Mafuele baada ya kukorofishana wakiwa nyumbani kwao kola hill mjini Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo ameeleza msichana huyo alimnyonga mtoto huyo baada siku ya jumatano baada ya kutokea mabishano kati ya marehemu na mtuhumiwa marehemu akimtuhumu dada yake kumuibia sox za shule huku akimlushia maneno ya kejeli ndipo mtuhumiwa akachukua uamuzi wa kumsukuma marehemu ambapo baada ya marehemu kudondoka sakafuni mtuhumiwa alimbeba kumpeleka chumbani na kumnyonga kwa kutumia kamba ya gauni na kusababishia kifo chake.
Nao wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia tukio hilo wametupia lawama baadhi ya wazazi kuwanyanyasa ndugu zao ambapo wamesema wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha wanawalea watoto kwa kuzingatia haki sawa ili kuepusha mauaji na unyanyasaji usiokuwa wa lazima.