Nape Amtaka Zitto Ajenge Upinzani wa Kweli.....Asema Akitaka Heshima Aachane na Siasa za UPINZANI Zenye Mlengo wa Kuruga Amani


Siku chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza kujiunga na  chama cha ACT-Tanzania, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amemtaka kujenga upinzani wa kweli kwa ajili ya kujenga  nchi na si kubomoa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Nape alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo upya katika ulingo wa siasa.

Alisema kinachotakiwa ni upinzani wenye lengo la kujenga na Zitto akitaka heshima aachane na siasa za Chadema zenye lengo la kuvuruga.

Hata hivyo, alisema hawawezi kuwa na mfumo wa vyama vingi vyenye lengo la kubomoa, hivyo ajenge upinzani wa kweli wa kuijenga nchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo