Mtoto
Mlemavu wa ngozi Albino Baraka Cosmas Lusambo,mwenye Umri wa miaka sita
Mkazi wa kijiji cha Ikonde kata ya Kipeta Sumbawanga vijijini Mkoani
Rukwa,amekatwa kiganja chake cha mkono wake wa kulia na watu
wasiojulikana,Lakini baba Mzazi Cosmas Lusambo anashikiliwa na
Polisi.Mtoto ameletwa Rufaa Mbeya jioni Ya jana.(Picha kwa hisani ya Henry Mdimu Balozi wa kijitolea wa kampeni ya ‘Imetosha’).
====== ====== ===== ======
Mtoto Baraka Cosmas Rusambo mwenye
umri wa miaka sita mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism), amekatwa mkono
wa kulia katika tukio lilitokea Jumamosi usiku tarehe7 Machi kwenye
kijiji cha Kiseta, Kata ya Kiseta, Tarafa ya Kiseta wilayani Sumbawanga
vijijini, mkoani Rukwa.
Baraka amepelekwa hospitali huku mama yake mzazi Bi. Prisca Shabaan amejeruhiwa vibaya wakati akijaribu kumlinda mwanae.
Jeshi la polisi linawashikilia watu wa wawili huku upelelezi ukiendelea.
Kwa taarifa zaidi za kina zitaendelea kuwajia kupitia mtandao huu