Kila kukicha kumekuwa na mambo mapya katika jamii inayotuzunguka na
kutokana na utandawazi umetufanya tuone na kujua kila kinachoendelea
katika ulimwenguni huu wa sayansi na teknolojia.
Kwa sasa kumekuwa na mitindo mbalimbali ya fashion kama kwenye nguo,
makeup, viatu na kubwa zaidi kuhusu hii style mpya hapa mjini ya kila
mtu kuweka dread kwa namna yake, sasa mama moja wa makamo na raia wa
Ghana alitoa mpya baada ya nywele zake kuzivisha kondomu kwa
kuzifunga kama dreadlock