Kijana
mmoja kutoka Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete
aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeanza
kupuputika huku nyama za kidole hicho zikionekana kulika.
Kijana huyo Eric Buageng,
alisema iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani
akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole chake, akaanza kusikia
maumivu na pete hiyo ikaanza kumbana kidole.
Eric
amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake
ulikuwa ukitetemeka, akashindwa kuitupa pia, halafu akasikia sauti
ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu
kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anasikia sauti ikimwambia atoke
nje.
Jitihada zake zimeonekana kutokuwa na
matumaini yoyote kwenye mikasa inayomkuta kwenye pete hiyo, ameshaenda
Hospitali na pia kwa wachungaji na hakuna mafanikio yoyote huku
wakihisi kwamba pete hiyo ina uhusiano na masuala ya uchawi.