Hii
ni moja ya story iliyopata Headline kubwa Kenya, inahusu mapacha watatu
waliopata alama sawa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE
kwenye matokeo yaliyotangazwa Jumanne wiki hii.
Mapacha hao Abenego Bingi, Meshak Barongo na Shadrack Isangoma
walipata alama ya B- ambazo ni 55, 56 na 57, wamesema wanapenda sana
somo la kiswahili ambalo walifanya vizuri kwenye mtihani huo wa kitaifa.
Mama yao Bi Eugene Amoti
ambaye ni Mchungaji katika Kanisa la New Light Kisumu, anasema kuwa
mapacha hao walikuwa na viwango tofauti vya kufaulu kwa masomo yao, kila
wakati walikuwa wakipata alama tofauti.
Walimu wa Shule ya Kisumu Day wamesema wameshangazwa sana matokeo hayo ambayo wanayaona kama baraka kwa shule hiyo.