Siku
chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014
na Rais Jakaya Kikwete, chama cha NCCR mageuzi kimesema sera hiyo haina
manufaa yenye tija kwa wananchi bali sera hiyo imelenga uchaguzi mkuu
kwa kuwalaghai wapiga kura na sio kutekeleza yaliyomo ndani ya sera
hiyo.
Mwenyekiti wa NCCR mageuzi taifa Mh James Francis Mbatia
ameyabanisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
wakati akieleza masuala mbalimbali yaliyoanishwa ndani ya sera mpya ya
elimu ambayo imeandaliwa kwa muda wa miaka saba hadi kukamilika kwake na
kuzinduliwa Februari 13 mwaka huu na rais Jakaya Kikwete na kuanisha
mpango wa serikali wa kutoa elimu bure pindi sera hiyo itakapoanza
kutumika jambo ambalo amelieza kuwa ni kutendawili kisichokuwa na jibu
kamwe.
Kuhusu muda wa kipindi cha miaka saba kilichotumika kuiyandaa sera
hiyo hadi kukamilika kwake Mh Mbatia amesema ni muda mrefu umetumika
huku sera ikiwa imegubikwa makosa mengi ya uchapaji pamoja na kushindwa
kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya sasa duniani hivyo sera
imeshapitwa na wakati hata kabla haijaanza utekelezaji wake kwa
wananchi.