Mwanamke mmoja ameieleza mahakama ya
nchini Kenya kwamba alilazimika kumuuza mtoto wake wa siku tano kutokana
na umaskini wa kupindukia ambao ulisababisha kukosa fedha za kumtunza
mtoto huyo.
Mama wa mtoto huyo Virginia Mwangi aliiambia Mahakama ya Nyeri kwamba alilazimika kumuuza mtoto huyo Shilingi 7,000 kwa Eunice Wangeci Kibira ambaye pia alishtakiwa kwa kosa hilo.
Wanawake hao wawili wanakabiliwa na
mashtaka manne ya kushirikiana katika biashara ya kumuuza mtoto huyo
kinyume na sheria ya watoto.
Mwangi alikiri makosa hayo mbele ya mahakama hiyo lakini Wendi alikanusha mashtaka na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi 50,000.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi