Baadhi
ya vijana wanaojihusisha na uchimbaji mchanga pembeni mwa mapango ya
mleni maji moto yanayodaiwa kuhifadhi makundi ya uhalifu, wamefanikiwa
kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa wa uhalifu kisha kumkabidhi kwa
vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Kamishna wa operesheni wa jeshi la polisi nchini afande Paul
Chagonja amesema baada ya kukamatwa kwa mmoja wa watuhumiwa jeshi la
polisi limefanikiwa kukamata silaha aina ya Shot gun pamoja na risasi 20
zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya shimo katika mapango.
Hata hivyo jeshi la polisi limewaomba wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwao kwa sababu jitihada za kukabiliana na uhalifu
zinaanzia kwa wananchi hivyo ni vyema wakaitikia wito ili hali ya
usalama iweze kuimarika.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaoishi eneo la Mleni maji moto
wameliomba jeshi la polisi kuimarisha hali ya usalama kwao baada ya
kumkamata mmoja wa wahalifu na kumkabidhi kwa vyombo vya dola kisha
kuishauri serikali kuchukua eneo lililoingiliwa na makundi hayo
yanayoitwa na jeshi la polisi kuwa ni majambazi kisha kuwamegea wananchi
wanaohangaika maeneo ya kilimo ili waweze kulima mazao ya chakula
badala ya kufuga vichaka ambavyo vimesababisha kuwa pango la uhalifu.