MAZISHI YA FAITH CATHERINE GONDWE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

Umati mkubwa wa waombolezaji wamejumuika na familia ya Mzee Geofrey Gondwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Marehemu Faith Catherine Gondwe, dada yetu aliyeaga dunia ghafla Jumanne iliyopita nyumbani kwao Baahari  Beach jijini Dar es salaam. Ujumbe wa sauti wa kurekodiwa kutoka kwa Mzee Gondwe ambaye yuko India kwa matibabu kuliwaliza wengi na wakati huo huo uliwafariji pale aliposema "Kufariki dunia kwa Faith ni mapenzi yake Mungu"
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Shada maalumu kwa Faith.
Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe, Profesa Amandina Lihamba akiweka shada la maua kwa niaba ya familia yao ambao ni ndugu wa karibu na familia ya Gondwe.
Wanachama wa Jambo Group ambao ni marafiki wa karibu wa baba wa marehemu wakiweka maua kaburini.
Marafiki waliosoma na Marehemu Faith nchini India wakiweka maua kaburini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo