Ni simanzi na majonzi katika kijiji cha Ndami, wilayani Kwimba ikiwa
ni siku 40 sasa, tangu mtoto Pendo Emmanuel (4), atekwe na watu ambao
hawajajulikana hadi sasa.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Mwandu Madirisha,
anasema wananchi wake hawapo vizuri kiakili tangu aibwe mtoto Pendo na
kwamba “hawaamini kama mtoto yule hajaonekana mpaka leo.”
Anasema kijiji hicho kina barabara kuu tatu zinazoingia na kutoka
katika vitongoji vya Misasi, Nyahonge na Chibwiji, hali inayochangia
kuwapo na ulinzi wa jadi (sungusungu).
Pendo, hakuna aliyefahamu wala kuhisi chochote kwani tumezoea kuishi kwa amani kwa miaka mingi,” anasema.
Mwenyekiti huyo anasema inawezekana watu hao walitumia hali hiyo
kufanya ‘uhalifu’ wa kuvamia nyumba yao iliyopo mbali kidogo na barabara
zinazolindwa na sungusungu.
“Naamini ni tukio la imani za
kishirikina linalowahusu zaidi wafanyabiashara wa migodini pamoja na
baadhi ya viongozi wa serikali ambao wanahitaji madaraka,” anasema.
Mama mzazi wa Pendo, Sophia Juma, ambaye kwa sasa amehamishwa katika
makazi yake na kupelekwa wilayani Misungwi, hakuwa na mengi ya kusema
kutokana na kumfikiria mtoto wake.
“Namkumbuka sana mwanangu, sielewi
huko alipo kipi kimemtokea, lakini namwamini Mungu waliotenda jambo
hilo, uso wa Mungu utawaumbua:-Sophia.