Mitandao ya picha na video za ngono CHINA nomaaaaaa

China Cyber
China na Sheria zao, Serikali ya nchi hii ni moja kati ya chache ambazo zimekuwa mstari wa mbele kwenye utekelezaji wa chochote kile ambacho watakiamua, kwa wakati wowote na kwa njia yoyote.

Moja ya stori za mwisho mwisho kusikika kutoka China ni ishu ya kila mtu kutakiwa kujisajili kwenye mitandao ya kijamii kwa majina yote halali yani, yale ambayo yanatambulika kwenye cheti cha kuzaliwa au passport hivi.

Kuna hii nyingine ya kuhusu hiyo hiyo mitandao, unaambiwa Mamlaka ya Mawasiliano China wamefuta website 65 ambazo watu walizitumia kwa masuala ya mapenzi ikiwemo kutafuta wapenzi na kushare picha za ngono.

Mitandao hiyo iligundulika kwamba watu walikuwa wakijisajili kwa majina fake, halafu wanashare picha, video za ngono pia.

Rungu limeanza kazi ndani ya China, yeyote anayetaka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii lazima ajisajili kwa jina lake kamili, hii itakuwaje mfano ikianza Bongo kwa kasi hii hii mtu wangu!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo