Watu
wawili mkoani Singida wamekufa na wengine zaidi ya ishirini na tano
wamejeruhiwa kwa kuvunjika mikono na miguu katika ajali mbili tofauti
zilizo husisha basi na lori na nyingine mwendesha pikipiki kugongwa na
lori.
Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida ACP Thobiasi Sedoyeka
amethibitisha kutokea kwa ajali hizo ambazo zimehusisha basi la Ngumuo
lenye usajili wa namba T 476 CSH aina ya yutong lilikuwa likitokea Moshi
na kuelekea Kahama na lori namba T 343 DCP lenye tela namba T 936 DBY
lilokuwa likitokea mwanza na kuelekea Dar-es-Salaam na kusema kuwa
zimesababishwa na mwendokasi wa dereva wa basi na uzembe wakati
akiendesha.
Wakielezea jinsi ajali ilivyo tokea majeruhi wamesema dereva wa
basi lao alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi huku mvua ikinyesha na
ghafla wakaona basi lao linayumba na kugongwa na tela la lori kisha
likapunduka mara tatu.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida
Daktari Daniel Tarimo amesema wamepokea maiti mbili na majeruhi ishirini
na sita ambao wamesha patiwa matibabu na wengine itabidi wapewe rufaa
ya kwenda hospitali KCMC na Muhimbili kwa sababu wamevunjika vibaya.