ZITTO KABWE AIBUA MAPYA BUNGENI, AGOMA KUSOMA RIPOTI YA PAC, KISA "KIPIGO" CHA PROF.LIPUMBA


Wakati  wa  Vurugu  za  Asubuhi  JANA  Bungeni, Spika  wa  Bunge  alimtaka  Mwenyekiti wa  PAC, Mh Zitto  Kabwe  aende   kusoma  taarifa  ya  kamati yake....

Kilichotokea  ni  kwamba, Zitto  alitia  mgomo, nikiwa  na  maana  kwamba  alipuuza  agizo  hilo  na  hakunyanyuka  kabisa. 
 
Unajua  ni  kwa  nini? Zitto  Kabwe  mwenyewe  amekwisha  lijibu  hilo  swali  kupitia  ukurasa  wake  wa   Facebook. 
"Kwa  nini  sikwenda  kusoma taarifa  ya  PAC leo  nilipoitwa  na  Spika? Jibu rahisi  kabisa, siwezi  kuona madhila na uvunjifu  mkubwa  wa  HAKI  za  binadamu  nikaendelea  na  mambo  kama  hakuna  kilichotokea.Kitendo  cha  polisi  kutumia  nguvu, kupiga  raia  hovyo  na  kumdhalilisha  kiongozi  wa CUF, Profesa  Ibrahim Lipumba  ni  kitendo  cha  kulaaniwa  kwa  nguvu  zote"- Zitto Kabwe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo