
TAARIFA zilizotufikia ni kwamba Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim
Lipumba na wanachama wake wamekamatwa na kupigwa na Jeshi la Polisi.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kushtushwa na
tukio hilo la kupigwa na kukamatwa Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof.
Lipumba.
Uongozi wa juu wa Chadema pamoja na mawakili wa chama hicho
wameelekea Kituo Kikuu cha Polisi, Dar kwa ajili ya tukio hilo
walilofanyiwa viongozi hao wa CUF na wanachama.
Juhudi za Mtandao huu kumpata Kaimu wa Kamanda wa polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, Afande Sirro zinaendelea baada
ya kumpigia simu hapo awali na kuomba kupigiwa baadaye kutokana na
kikao alichokuwa nacho.