MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE AUAWA KWA KUPIGWA NA
WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA WIZI.
MTU MMOJA
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 30-35, ALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.01.2015
MAJIRA YA SAA 16:17 JIONI HUKO ENEO
LA MWANJELWA, KATA YA MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA
KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUTUHUMIWA
KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA UVUNJAJI LA TAREHE 26.01.2015. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE
TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]