Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Karangalala
ameamuriwa na mama yake kufanya hivyo baada ya mama yake Helena
kumwachia jukumu la kupika mboga Novemba mwaka jana lakini mboga hiyo
iliungua.
Baada ya kuunguza mboga hiyo,mama huyo alimpiga mwanaye kabla ya kumpa masurufia na kumkabidhi chumba tayari kwa kuanza maisha.
Mtoto huyo alisema mama yake amekua na tabia ya kumpiga mara kwa mara kiasi cha kusababisha mwili wake kuwa na alama za viboko.
“Sifahamu kwa nini mama yangu huwa ananipiga kiasi hiki,inawezekana
kwa kuwa na yeye alilelewa na mama wa kambo aliyekua anampiga
hivi”alisema mtoto huyo.