Serikali kuja na adhabu mbadala kwa makosa madogo ili kupunguza msongamano Magerezani


Serikali ya Tanzania imesema ipo kwenye mchakato wa kuandaa adhabu mbadala kwa wahalifu wa makosa madogo madogo ili kupunguza msongamano magerezani ambao kwa sasa unapelekea hali mbaya katika Magereza hayo.
 
Akijibu swali bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi Bi. Celina Kombani amesema hali ya msongamano kwa sasa katika magereza inatokana na Majengo yake kuwa ni ya muda mrefu na yalikuwa yanatosheleza katika kipindi yalipojengwa.
 
Kombani amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa kuboresha Magereza hayo kwa bajeti iliyopo ila kwa sasa kitakachofanyika ni kutoa adhababu mbadala kwa wafungwa wenye makosa madogo madogo ikiwemo vifungo vya nje.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo