Rais
Jakaya M. Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo
Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya
kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena
hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na
ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais, Profesa Mohamed Janabi
Rais Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka hospitalini.
Habari picha kutoka kwa Freddy Maro/Ikulu.