Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Kanali mstaafu Issa Machibya akiongea na
waandishi wa habari(ambao hawapo pichani)ofisini kwake juu ya kusitisha
kwa zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi iliyotokea hivi
karibuni katika kijiji cha kalalangabo ziwa Tanganyika.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
SEREKALI ya Mkoa wa Kigoma imesitisha zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi miwili ya maharusi iliyotokea tokea hivi karibuni katika Ziwa Tanganyika kwenye kijiji cha Kalalangabo kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika .
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa vikosi mbalimbali vya ukoaji kwa kushirikiana jeshi la wananchi (JWTZ) wakishirikiana na wananchi wamefanya kazi kubwa sana ya kuopoa miili kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.
Alisema jumla ya miili kumi ili patikana katika zoezi hilo la ukoaji lakini hivi sasa wameachia uongozi wa kijiji cha serekali ya kalalangabo kuendelea kutoa taarifa kama kuna miili mingine itakayoibuka.
''Ile mitumbwi ilikuwa imejaza sana watu ambayo idadi yake kamili mpaka sasa bado haijajulikana kwani walivyokuwa wanaenda kupanda walikuwa na haice tatu,pikipiki 10 na vyote vilikuwa ndugu jamaa na wapambe wa maharusi.
ili kuwa mitumbwi miwili ya kienyeji tena ile inayotumika kuvulia samaki na dagaa,sasa tunahofia kwamba miili mingine zaidi itakuwa bado ipo majini kwani jana waokoaji walifanikiwa kupata baadhi ya vitu majini kama vile simu,nguo na saa''alisema Machibya.
Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutumia vyombo visivyo rasmi katika usafiri na ambavyo havijasajiriwa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini(SUMATRA)pia aliwataka wavuvi na wale wenye vyombo majini waache tabia ya kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi ya kuvulia dagaa ili kuepuka ajali.
Pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya majini wote wasajili vyombo vyao na wahakikishe vinaanzia safari katika vituo vinavyotambulika.
''Kuna siku mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tunaingia majini wenyewe kufanya ziara ya ghafla siku nzima na kuwakamata wale wote wanaokiuka sheria za kusafirisha abiria ziwani''alisema Machibya
Machibya alisema kuwa mmiliki wa mitumbwi hiyo bado hajafahamika vyombo vya usalama bado vinaendelea na juhudi kumtafuta mmiliki wa mitumbwi hiyo ili aweze kufikishwa katika sheria