Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas
Kiongozi
wa matukio
ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa
jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa
akijaribu kukimbia.
Akithitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani
Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo
limetokea October 19 majira ya saa tano na nusu katika
barabara ya babati mkoani Arusha
wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.
Alisema kuwa
mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki
mbili zilizopita huko mkoani
Morogoro mara baada ya kutafutwa kwa
muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani kondoa mkoani
Dodoma kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo
alikuwa ameficha mabomu mengine.
"mtuhumiwa huyu
alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila
mafanikio kwani alikuwa akai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani
morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyia mahojiano
alisema ameficha mabomu mengine huko kondoa na jana alikuwakipelekwa kuonyesha
ndipo alipotumia trikizake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga gudo na
kutaka kuwakimbia askari ndio akapigwa risasi mbili"alisema
Sabas
Alitoa wito kwa
wananchi kuendelea kuwafichua waovu ili kuwaza kuteketeza
matukio ya uhalifu
habari kwa mujibu wa woindeshizza blog