Rais wa jamhuri ya muungano wa
tanzania Mhe.Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuwa
wavumilivu wakati serikali inapoandaa mchakato wa kura ya maoni juu ya
katiba iliyopendekezwa, huku akiwatahadharisha vijana kutotumika kwa
masilahi ya wengine, bali waangalie mstakabali wa maisha yao na malengo
ya katiba.
Mhe. Rais ametoka kauli hiyo mkoani Tabora katika kilele cha mbio za
mwenge wa uhuru, sambamba na kumbukumbu ya miaka 15 ya kifo cha muasisi
wa taifa la Tanzania hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambapo amesema kuwa, katiba inayopendekezwa ilelenga kutatua
changamoto za vijana.
Aidha akizungumzia kudumisha mbio za mwenge wa uhuru, mhe. Rais
amesema kuwa, watanzania wataendelea kuwasha na kukimbiza mwenge wa
uhuru unaowaangazia hata nchi jirani kwani uhuru wa nchi hizi
umepatikana kwa namna moja ama nyingine kutokana na amani iliyopo hapa
nchini, kutokana na baadhi ya viongozi wake kuhifadhiwa hapahapa nchini.
Aidha akizungumza kabla ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa
wakimbiza mwenge kitaifa, waziri wa Habari, utamaduni vijana michezo mhe.
Fenera Mkandala amesema kuwa, mwenge wa uhuru umekimbizwa kwa mafanikio
ambapo miradi ya maendeleo 1451, yenye thamani ya zaidi ya shilingi
bilioni 361, imezinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi.
Kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge
wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya
kilele cha mbio za mwenge ulius na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan
Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na
michezo Dkt.Fenela Mkangara.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenge wa Uhuru wakati wa
maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ziizofanyika mkoani Tabora leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kilele
cha mbio za mwenge 2014 ziilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora leo(picha na Freddy Maro)