NA KENNETH NGELESI,MBEYA
MBUNGE wa jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi
amesema kuwa kuna haja kwa Serikali kungalia namna ya kuondoa ushuru katika
vifaa vinavyo ingia nchini kwa ajili ya masuala ya tiba mbadala kwani wanao
nufaika na vifaa hivyo ni wananchi wa kawada.
Rai hilo ilitolewa
juzi jijini hapa na Mbunge huyo wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja
Tangu kituo cha (LITECH) kinacho jihusisha na masauala ya tiba mbadala kwa kutumia vifaa, kwa magonjwa yasiho
ambukizwa kilichopo eneo la Block ‘T’ jiji hapa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo yeye alikuwa mgeni
rasmi Mbilinyi alisema kwa kutokana na taarifa ya kituo hicho ambapo tangu
kianze kutoa huduma kwa zaidi ya mwaka mmoja kimekuwa kikihudumia wagonjwa 500
kwa siku, ni wazi kituo hicho kinatoa huduma bora kwa jamii hivyo kuna kila
sababu kwa Serikali kukiunga mkono kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo vinavyotumika kwa ajili ya
tiba mdala kwa maradhi mbalimbali.
Mbilinyi alisema kituo hicho kinapaswa kuungwa Mkono na
jamii ya Kitanzania kwani licha ya asili yake ni Korea kusini lakini watu walioajriwa
na kutoa huduma ni wazawa tofauti na makampuni mengine ya kigeni ambayo mara tu
yanapo pata kibali cha kutoa huduma yeyote
hapa nchi yamekuwa na kasumba ya kuleta watu wao kwa ajili ya kufanya shughuli
mbalimbali hata zile ambazo zingeweza kufanywa na wazawa.
‘Uamuzi wa kituo
chenu kuajiri wazawa ni jambo kujivunia
kwani uzoefu unaonyesha kuwa makampuni mengi nchini yakisha pata kibali cha
kufanya kazi wanakuja na watu wao jambo si zuri kwa nchi yetu “alisema Sugu.
Alisema kuwa kitendo cha kuajiri wazawa kinongeza ufanisi
katika kazi kwani wagonjwa pamoja na wahudumu wanaongea lugha moja jambo ambalo litaongeza ufanisi katika kituo
hicho.
Hata hivyo Mbunge alisema kuwa ni vema kituo hicho kikapunguza gharama za matibabu ili kila mtu hasa wale
wenye kipato cha chini ili waweza kumudu kwani maradhi hayo yanamkumba kila mtu
pia kpunguza gharama za kitanda ambapo
kimekuwa kitumika kwa ajili tiba pamoja na mazoezi.
Awali akisoma taarifa mbele ya Mbunge huyo Mkurgenzi wa Tasisi hiyo
Dk Joseph Rema alisema kuwa maradhi yasiyo ambukizwa hapa nchi yanasababishwa na uti wa mgongo kutokana na
kuwa mfumo wa mawasilianoi katika mwili unanzia kwenye uti mgongo.
Alisema kuwa mbali na
kituo cha Mbeya lakini Tasisi hiyo yenye asili ya Korea Kusini kwa hapa
Tanzania ofisi kuu zipo mjini Morogoro na kwamba imeshafungua vituo kama hicho
katika Mikoa Dar-ees-salaam,Mwanza na Tunduma.
Katika hatua nyingine Dk Rema alibanisha magonjwa ambayo si
ya kuambukizwa na wanachi wengi wamekuwa wakifika katika vituo vyao kwa ajili
ya kupata tiba kuwa, Kansa, Vitonda vya Tumbo,Uvimbe kwenye Kizazi,Kiharusi, na
Magonjwa mbalimbali ya Uzazi.