Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene
akizungumza na viongozi na watendaji wa Manispaa tatu za Jiji la Dar es
Salaam kuhusu maagizo ya namna ya kusimamia maeneo ya wazi. Pia, ametoa
siku 14 kuanzia jana Alhamisi kwa Manispaa hizo kubomoa maeneo ya wazi
yaliyovamiwa ambayo yalikwishatolewa Ilani. Aidha, Naibu Waziri ametoa
siku 30 kwa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha ofisini kwake utaratibu
wa namna ya kusafisha fukwe.
Watendaji
wa Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalam wa
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene
kuhusu namna yak usimamia maeneo ya wazi jijini Dar.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene
(katikati) akitoa maagizo ya usimamizi wa maeneo ya wazi jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Temeke Bw. Maabad Hoja na Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Khery Kessy.(Picha zote na Rehema Isango)