MAJERUHI WA AJALI YA LORI LA MAFUTA MBAGALA WAZIDI KUFARIKI DUNIA

Idadi ya watu waliokufa kufuatia ajali ya moto iliyotokana na kulipuka kwa tanki la mafuta la lori lililopinduka Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam imeongezeka hadi  kufikia saba.
 
Aidha, hali za majeruhi tisa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mbaya.
 
Idadi ya vifo imeongezeka baada ya majeruhi waliokuwa wamelazwa MNH  wawili kufariki  dunia usiku wa kuamkia jana.
 
 Afisa habari Msaididizi wa MNH, Doris Ishenda, alithibitisha kufariki kwa watu hao Nurdin Mazinga (22) na Abas Hugangar, wakazi wa Mbagala.
 
 “Usiku wa kuamkia Jumanne tulipokea majeruhi 15 kutoka Hospitali ya Temeke ambao kati yao sita wameshafariki dunia,” alisema na kuongeza kuwa miili yao  imehifadhiwa hospitalini hapo.
 
Watu 20 waliungua vibaya  sehemu mbalimbali za miili na mmoja kufariki dunia papo hapo  baada ya kulipukiwa na petroli wakati  kundi la vijana walipokuwa wakijaribu kupora mafuta  kwenye lori hilo  lilopinduka  eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii usiku.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo