Aliyekuwa
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mtera,
Lameck Lubote ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na kusema amechoka na siasa zilizojaa udikteta wa
viongozi wake.
Alisema
amekerwa na kuingizwa kwa udini katika siasa kwa kuwashirikisha
maaskofu wenye mwelekeo wa Chadema kwa kusingizia Jukwaa la Kikristo.
Alisema
hayo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa jana huku akiwa amefuatana
na mwanachama mwenzake ambaye naye amehama Chadema, Gwakisa Mwakasendo.
“Nimechoshwa
na ninakerwa na siasa za kitoto zinazofanywa na Chadema pamoja na chama
hicho kuwa na maandamano yasiyokwisha,” alisema.
Pia
alisema viongozi ndani ya chama hicho wamekuwa na maamuzi ya kidikteta
ambayo yana maslahi ya wachache kitu ambacho si sawa sawa.
Lubote
alisema Chadema imejaa vituko ikiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho,
Freeman Mbowe kuhamasisha maandamano huku yeye akiondoka kwenda Afrika
Kusini.
“Lakini
jambo linaloonekana kuwa ni hatari zaidi ni kuingiza udini katika siasa
kwa kuwashirikisha maaskofu wenye mwelekeo wa Chadema kwa kusingizia
jukwaa la Kikristo,” alisema.
Alisema
jambo hilo lilisababisha maaskofu wenye mwelekeo wa Chadema kufikia
hatua ya kutoa tamko la upande mmoja lenye lengo la kuhukumu ambalo
lilikuwa limejaa chuki.
“
Hata tamko hilo halikufaa kusomwa makanisani kwa kuwa maudhui yake
yenye amri , kiburi na chuki hayafanani na mwelekeo wa Ukristo jambo
kama hili ni hatari sana” alisema.
Pia
alisema wamekuwa wakishuhudia kauli za utata za viongozi wa Chadema na
hata mkakati waliokuwa nao wa kuzuia kupatikana kwa Katiba umeshindwa
vibaya na kukisababishia Chama hicho aibu kubwa .
Alisema
katika maeneo mengi sasa chama hicho kimekuwa kikipuuzwa na kukejeliwa
kwa sababu hakuna maelezo kwa wanachama kuhusu mantiki ya kuendelea
kuzuia mchakato wa katiba.
Alisema
kugomea mchakato wa katiba si njia ya kuleta Serikali tatu na jambo
hilo linaonekana ni ukorofi wa baadhi ya viongozi wa Chadema
wanaong’ang’ania mkakati ulioshindwa wa kususa vikao vya kitaifa,
kuchochea maandamano, vitendo ambavyo vinaonesha kupenda fujo.
Aidha
alisema hivi karibuni wameshuhudia jinsi Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,
Samuel Sitta alivyoandamwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kashfa nyingi
katika magazeti kisa walitegemea angewalinda katika mambo yao yasiyo
faa kama vile kutaka serikali tatu kwa lazima.
Hata
hivyo, alibainisha viongozi ndani ya chama hicho wamekuwa wakidai
kupiga vita ufisadi huku wao wenyewe wakiongoza kukifanyia ufisadi chama
hicho.
Alisema baadhi ya viongozi wamekuwa wakidai kurejeshewa fedha walizokikopesha lakini hakuna mkataba unaonyesha makubaliano hayo.