DEREVA AMSHUSHIA KIPIGO KIBAKA ALIYENASA MLANGONI MWA BASI HUKU AKIENDESHA, ANGALIA VIDEO HAPA

Katika kituko hiki kilichotokea katika jiji la Concepción, nchini Chile, huyu kibaka, alipodaiwa nauli mara baada ya kuingia kwenye basi, alimwambia dereva kuwa hana nauli, na kuwa mmoja wa abiria ni shangazi yake (kitu ambacho si kweli.) Kisha akaanza kutoa visingizio kibao, akisubiri nafasi ya kukwapua pochi. 

Dakika ya mwisho, wakati basi linaanza kufunga mlango, alijaribu kukwapua mkoba wa mwanamke aliyekaa siti ya mbele. Bahati nzuri alishindwa kuiba mkoba huo, halafu alichelewa kutoka nje ya basi na kunaswa na mlango uliokuwa unajifunga. Hapo ndipo dereva alipotoa rungu lake na kuanza kumpa kichapo huku akiendelea kuendesha basi. 

Kibaka huyo aliendelea kula kichapo huku akijitetea au kuomba msamaha, mpaka basi liliposimama mbele ya askari polisi, na askari huyo kumtia mbaroni. Taarifa zaidi zinasema kuwa kibaka huyo ana historia ya uhalifu, na kwa sheria za nchi hiyo, ambazo ni kali kwa wahalifu wanaorudia makosa, ataishia jela.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo