Chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema kimesema kinajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa
utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu na haitosusia uchaguzi huo ili
kukabiliana na hujuma mbalimbali zinazofanywa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chadema jijini
Dar es Salaam katibu mkuu wa chama hicho Dr Willbroad Slaa amesema kamwe
hawatasusia uchaguzi huo kwani Tanzania ina vyama vingi vya siasa wao
kama Chadema pekee hawawezi kusitisha utaratibu wa uchaguzi na kwa
kufanya hivyo wataiachia CCM ushindi.
Naye mwanasheria mkuu wa chama hicho Tundu Lissu amesema chama
chake kinaungana na baadhi ya taasisi na viongozi wa dini kulaani
matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mchakato wa katiba tokea hatua
za awali mpaka upigaji wa kura unaoonekana kwenda kinyume, hivyo Chadema
inajiandaa kuanza kampeni ya kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi
kuipigia kura ya hapana rasimu ya katiba iliyopitishwa na Bunge.