Ajali kubwa ya moto ambao chanzo chake
bado hakijafahamika, imetokea na kuteketeza bweni la wanafunzi wa shule
ya Sekondari ya Mtakatifu Petro iliyopo eneo la Iwanzari, Tabora pamoja
na vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo.
ITV wameripoti kuhusiana na tukio hilo,
ambapo moto huo umezuka ghafla wakati wanafunzi wakiwa katika ibada na
hata baada ya taarifa kuwafikia askari wa kikosi cha zimamoto hawakutoa
ushirikiano wowote kwa madai kuwa magari ya kuzima moto ni mabovu
kitendo kilichowasikitisha mkuu wa shule hiyo Simon Kyala pamoja na
askofu wa kanisa hilo Mhashamu Elias Chakupewa.
Meya wa Tabora, Gulam Dewji na mratibu
mwandamizi mkuu wa kikosi cha zimamoto Tabora, Kondo Mwamed wamesema
manispaa ina gari moja na liko katika matengenezo kwa takribani miezi 2.
Thamani ya vitu vilivyoteketea bado
haijafahamika japo mkuu wa shule amekiri kuwa wanafunzi hao wameathiriwa
na janga hilo kipindi ambacho wanakaribia kuanza mitihani